MICHAEL Carrick ameumia enka na atakuwa nje ya uwanja kwa wiki 10 hadi 12, kocha mpya wa Manchester United Louis van Gaal amefichua.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32 alifanyiwa upasuaji Alhamisi asubuhi na sasa atakosa mwanzo wa kampeni za msimu ujao.
Louis van Gaal amesema hilo ni pigo kwa kikosi chake kwa vile Michael Carrick ni mchezaji mzoefu.
"Siku zote ni muhimu kuwa na wachezaji wazoefu, lakini sio kwa umri tu, sio kwa uzoefu wa soka tu, bali pia kwa uzoefu wa mambo ya kibinadamu," alisema Van Gaal.
Taarifa rasmi ya klabu imesema: "Michael Carrick amefanyiwa upasuaji wa enka yake ya kushoto na atakuwa nje ya uwanja kwa wiki 10 hadi 12."