Sunday, July 06, 2014

KANISA LA TAG (TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD) LAKABIDHI MSAADA WA VYANDARUA 1300 KWA HOSPITALI NA VITUO VYA AFYA MKOANI RUKWA



KANISA LA TAG (TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD) LAKABIDHI MSAADA WA VYANDARUA 1300 KWA HOSPITALI NA VITUO VYA AFYA MKOANI RUKWA
Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Jimbo la Rukwa Mchungaji Nestory Watua akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Methew Sedoyyeka vyandarua 1300 vya kukinga mbu waenezao Malaria kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya tarehe 04/07/2014. Msaada huo ni sehemu ya vyandarua 8550 vitakavyotolea na Kanisa hilo kwa Mikoa ya Mbeya, Njombe na Rukwa katika kuadhimisha  Jubilee ya miaka 75 ya Kanisa hilo nchini. Pamoja na zoezi la ugawaji vyandarua hivyo maadhimisho hayo yataenda sambamba na zoezi la uchangiaji damu na huduma mbalimbali za kiroho.
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Methew Sedoyyeka akizungumza katika hafla hiyo fupi ya makabidhiano ambapo amelishukuru kanisa hilo kwa mchango walioutoa wa kuunga mkono juhudi za Serikali katika mapambano dhidi ya malaria. Ameziomba taasisi zingine binafsi kuiga mfano huo kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuleta maendeleo hapa nchini. Katika hatua nyingine amepiga marufuku matumizi mabaya ya vyandarua ikiwemo tabia ya kuzungushia kwenye bustani za mbogamboga ambapo amezitaka mamlaka husika kuwakamata watu wa aina hiyo na kuwachukulia hatua kali kutokomeza tabia hiyo.
Muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya katika hafla hiyo fupi ya makabidhiano Ndugu Methew Sedoyyeka ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga akizungumza katika hafla hiyo ambapo amewataka viongozi wa Serikali na wananchi kuhamasishana kwenye shughuli za usafi na uhifadhi wa mazingira ili kutokomeza mazalia ya mbu waenezao Malaria na ugonjwa hatari wa Dengue. 
Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Jimbo la Rukwa Mchungaji Nestory Watua akizungumza katika hafla hiyo muda mfupi kabla ya kukabidhi vyandarua 1300 kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa tarehe 04/07/2014. Alisema kuwa Kanisa la TAG lilizaliwa Igale Mkoani Mbeya mwaka 1939 na sasa  linaadhimisha Jubilee ya miaka 75 ambapo kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni "Mungu anajali roho yako na mwili wako, jenga mahusiano nae"
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. Mtika akifanya utambulisho wa wenyeji katika hafla hiyo.
Vyandarua 1300 vilivyokabidhiwa kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa na Kanisa la TAG, vyandarua hivyo vitagawiwa katika hospitali, vituo vya afya na zahanati zilizoainishwa Mkoani Rukwa. 
Picha ya pamoja.