Sunday, July 20, 2014

Dkt. Magufuli asema Wilaya ya Nyasa - Mbinga kuunganishwa kwa kwa Barabara ya Lami



Dkt. Magufuli asema Wilaya ya Nyasa - Mbinga kuunganishwa kwa kwa Barabara ya Lami
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John P. Magufuli, (Mb) amesema kuwa Serikali itajenga barabara kwa kiwango cha lami kuunganisha Wilaya ya Mbinga hadi Mbamba bay Wilaya mpya ya Nyasa itakayokuwa na urefu wa Kilometa 67.

Dkt. Magufuli aliyasema hayo jana alipokuwa anahutubia mamia ya Wakazi wa Nyasa kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa mpira wa miguu Mbamba bay, mara baada ya Mheshimiwa Rais Jakaya Kiwete kufungua Madaraja pacha ya Ruhekei A, B na C yaliyogharimu kiasi cha Tsh. bil.4.

"Mhe. Rais napenda kutamka hapa kuwa kama tumeweza kujenga mtandao wa barabara za lami zaidi ya km. 11,000 nchi nzima hatuwezi kushindwa kujenga km. 67 kwa kiwango cha lami.

Waziri Magufuli aliongeza kuwa tayari Wizara ya Ujenzi imetenga fedha kiasi cha Shilingi Bil. 2.3 katika mwaka wa fedha 2014/15 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara hiyo katika kiwango cha lami.
Umati wa wananchi wa Wilaya ya Nyasa waliokusanyika kwenye mkutano wa hadhara kumsikiliza Mhe.Rais Jakaya Kikwete.
Mhe. Dkt. John P. Magufuli akiongea na wananchi wa Wilaya ya Nyasa hawapo pichani kwenye kwenye mkutano wa hadhara mjini mbamba bay jana.
Rais Jakaya M. Kikwete akipita juu ya daraja la Ruhekei mara baada ya kulifungua rasmi pembeni yake ni Waziri wa Ujenzi Mhe. John P. Magufuli.
Waziri wa Ujenzi Mhe. John P. Magufuli na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe wakiwa na furaha walipokutana kwenye sherehe za ufunguzi rasmi wa daraja la Ruhekei.
Raia wa nchi za kigeni nao hawakuwa nyuma kuja kujumuika na wananchi wa Nyasa kwenye mkutano huo wa hadhara.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Tanroads na Wizara ya Ujenzi makao makuu wakishiriki kwa pamoja katika sherehe za uzinduzi wa daraja la mto Ruhekei.