Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi Balozi Seif Ali Iddi amewathibitishia Wana CCM, Wananchi na Jamii kwamba ataendelea kufuatilia matatizo na changa moto zinazowakabili wananchi popote pale akiwa kama mtendaji Mkuu wa Serikali.
Alisema Wanasiasa wasifikirie kwamba anapokwenda majimboni hasa katika maeneo yanayoongozwa na Upinzani wakadhani ya kuwa anakwenda kuvuruga siasa za vyama vyengine vya upinzani.
Balozi Seif alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Wana Maskani ya CCM ya Amani na Utulivu iliyopo katika Kijiji cha Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja akitekeleza ahadi waliyoitoa yeye na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dr. Ali Moh'd Sheni katika ziara yao ya Tarehe 2 Mei Mwaka 2013 ya kujenga Maskani hiyo katika hadhi ya kisasa.
Akikabidhi mchango wa shilingi Milioni 4,000,000/- zitakazotumika katika ujenzi wa Maskani hiyo Balozi Seif alisema bado ana wajibu wa kufanya hivyo kwa vile yeye ni kiongozi wa Serikali na Siasa.
Alifahamisha kwamba anachokifanya muda wote ni kuangalia shida na kero zinazowakabili Wananchi na kutafuta mbinu za kuzikwamua na zile zilizo nje ya uwezo wake huziwasilisha Serikalini kwa hatua zaidi ya kutafutiwa ufumbuzi muwafaka.
Aliwashangaa baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaoendelea kumshutumu kwa kitendo na uamuzi wake wa kufuatilia kero, matatizo na changamoto hizo zinazowakabili wana jamii katika maeneo yao mbali mbali hapa Nchini.
Naye Mke wa Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Mama Asha Suleiman Iddi aliwatanabahisha akina mama wa Vijiji hivyo kujiepusha na ushawishi wa vurugu za wanasiasa ambazo maafa yanayotokea huwapata wanawake na watoto.
Mjumbe Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wanamaskani ya Amani na Utulivu Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Balozi Seif akimkabidhi fedha Taslim Shilingi Milioni 4,000,000/- Mwanachama wa Maskani ya Amani na Utulivu ya Nungwi Bibi Leila Kheir Haji kwa ajili ya ujenzi wa maskani yao ikiwa ni utekelezaji wa ahadi waliyoitoa na Rais wa Zanzibar.
Baadhi ya Akina Mama wa Kijiji cha Mvuleni Kidoti wakitoka ndani ya pango kujipatia huduma za maji safi wakishuhudiwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Balozi Seif aliyetembelea kijiji hicho.
Balozi Seif akikagua Msikiti wa Ijumaa wa Kijiji cha Mvuleni ambao unahitajika kunyanyuliwa ili kutoa hufrsa nzuri kwa waumini wa dini ya Kiislamu kufanya ibadaza yao kwa utulivu.Kulia ya Balozi Seif ni Imamu wa Msikiti huo Sheikh Khamis Duchi Kheir na kushoto yake ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Nd. Haji Juma Haji.
Balozi Seif akimkabidhi Seti ya Jezi Kijana Zamir Simai Haji kwa ajili ya Timu ya Vijana wa CCM wa Kijiji cha Mvbuleni kiliopo Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Katibu wa CCM Tawi la Nungwi Nd. Adibu Ali Sheha akitoa Taarifa fupi ya Maskani ya CCM ya Amani na Utulivu ya Kijiji hicho ambayo itajengwa kwa mchanga wa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar Dr. Ali Mohd Sheni kwa kushirikiana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi.
Baadhi ya wanamaskani ya amani na Utulivu ya Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja wakisikilizika Majumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif hayupo pichani aliyefika kwenye maskani hiyo kutekeleza ahadi waliyotoa na Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohd Sheni. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.