UMATI   WA WAKAZI WA KIJIJI CHA UCHUNGA WAKITAZAMA AJALI YA FUSO
    Watu 3 wamekufa na wengine   zaidi ya 47 wamejeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kwenda mnadani   kupinduka wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga.
Ajari   hiyo imetokea  asubuhi katika eneo la uchunga wilayani humo baada ya gari   hilo haina ya fuso namba T680 ARL kuacha njia na kupinduka.
  Chanzo cha ajari hiyo ni   mwendo kasi na derava wa gari hilo aliyetambulika kwa jina la Shija Ngassa   amekimbia  baada ya ajari hiyo
  Ajari   hiyo ya fuso imesababisha vifo vya watu watatu ambapo moja ametambulika kwa jina   la Difa Shimo  mili ya marehemu imehifadhiwa kwenye hospitali ya mkoa wa   Shinyanga.
  Kamanda   wa polisi wa mkoa wa Shinyanga kamishina msaidizi wa polisi Jastus Kamugisha   amethibitisha kutokea kwa ajari hiyo.
  Kamugisha   amesema jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo pamoja na kumsaka   dereva wa gari hilo sanajali na kutoa onyo kwa wafanya biashara wa minadani   kuacha kupanda magari ya   mizigo


 
