Monday, June 30, 2014

TIMBWILI LA KUSHIKANA UCHAWI LATIKISA


TIMBWILI LA KUSHIKANA UCHAWI LATIKISA
Mzee Kikongwe aliyefahamika kwa jina moja la Siberi anayetuhumiwa kwa ulozi.Katika hali ya kushangaza, mama aliyetajwa kwa jina la Khadija Omari amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kushikana uchawi na kikongwe anayefahamika kwa jina moja la Siberi akiwa na mganga wake, Rashid na kuibua timbwili lililotikisa, akimtuhumu kikongwe huyo kumchukua mwanaye kimazingara 'msukule'.Tukio hilo lilitokea wikiendi iliyopita maeneo ya Mgeni-Nani, Mbagala jijini Dar na kusababisha sekeseke kubwa lililofunga mtaa kufuatia mvutano ulioibuka baina ya wakazi wa mtaa huo huku baadhi wakiamini ushirikina wakimhusisha kikongwe huyo.

Mama aliyetajwa kwa jina la Khadija Omari anayemtuhumu mzee huyo.
Kwa mujibu wa Khadija ambaye ni mama mzazi wa mtoto anayedaiwa kuchukuliwa msukule aitwaye Tausi, mwanaye huyo alifariki dunia Agosti, mwaka jana katika mazingira ya kutatanisha.
Alisema kifo cha mwanaye kilimtatiza hivyo alikwenda kwa waganga wa jadi 'kuchungulia' kama alifariki dunia kweli au ni mauzauza ndipo akabaini kuwa kikongwe huyo ambaye alikuwa mwenye nyumba wake anahusika.

Mganga akijaribu kutoa dawa ya kurejesha mtoto.
Kufuatia hali hiyo, Khadija aliamua kuondoka kwenye nyumba ya kikongwe huyo kwani alikuwa akikutana na mauzauza kila kukicha na kutimkia mkoani Mwanza huku akijipanga kutafuta mtaalam wa kumtoa mwanaye alipowekwa msukule.
Alisema hivi karibuni alirejea Dar na kutinga kwa kikongwe huyo akiwa na waganga wa jadi ili kumpata mwanaye.

Baadhi ya mashuhuda waliofika kushuhudia sekeseke hilo.
Hata hivyo, zoezi hilo halikufanikiwa baada ya ndugu wa kikongwe huyo kuingilia kati na kuanzisha timbwili la aina yake wakimtetea kwa madai hawana imani kama anajihusisha na vitendo vya aina hiyo.