Meneja wa NMB kanda ya kaskazini Vicky Bishubo akimkabidhi ripoti ya wanahisa kamanda wa polisi mkoani Arusha Liberatus Sabas katika hafla ya kukabidhi pikipiki kwa jeshi hilo ofisini kwa kamanda sabas makao makuu ya jeshi hili mkoani Arusha.
Mahmoud Ahmad-Arusha
Jeshi la polisi limepokea msaada wa pikipiki mbili kutoka kwa benki ya NMB katika hafla iliyofanyika makao makuu ya jeshi hilo na kuhudhuriwa na askari mbalimbali akiwemo mkuu wa upelelezi mkoa,afisa mnadhimu wa jeshi hilo mkoani hapa na wafanyakazi wa benki ya nmb.Hafla hiyo ya makabidhiano ilienda sambamba na kukabidhi taarifa ya gawiwo la mwaka la wanahisa lililokabidhiwa kwa kamanda wa polisi kamishna msaidizi wa polisi Liberatus Sabas na meneja wa benki ya NMB kanda ya kaskazini Vicky Bishubo katika ofisi za kamanda huyoAkizungumza baada ya kukabidhiwa pikipiki hizo kamanda wa polisi mkoani hapa alisema kuwa pikipiki hizo zimekuja wakati muafaka na zitasaidia katika kuweka hali ya usalama na kuwaraisishia kufika maeneo ya tukio kwa uraisi hivyo wakilishukuru benki hiyo na kuitaka kutoishia hapo.
Nae meneja wa benki hiyo kanda ya kaskazini alisema kuwa wametoa pikipiki hizo ili kuweza kulisaidia jeshi hilo katika kuhakikisha usalama na ulinzi wa raia unaendelea kuimarishwa kwani hali ya usalama wa raia umeonekana kuimarika kwa siku za karibuni hivyo wakiwa kama wadau wetu tumeona kuwasaidia hichi kidogo tukijaa liwa tunaweza kuongeza zaidi.