Uholanzi 5 -1 Uhispania
Mabingwa watetezi wa kombe la dunia wameambulia kichapo cha mabao 5-1 mikononi mwa timu walioishinda katika fainali huko Afrika Kusini miaka minne iliyopita.
Kabla ya leo Uhispania ilikuwa haijashindwa katika dakika 476 ya mechi za kombe la dunia.
Mabao hayo ni zaidi ya mabao yote waliofungwa katika mchuano wa Euro na kombe la dunia la mwaka wa 2010 huko Afrika Kusini.
Je Umejifunza nini kutokana na kichapo hicho cha mabingwa wa Dunia ?
Taarifa zinazohusiana
23:40 Uholanzi 5-1 Uhispania dakika ni ya 90.
23:38 Robben anampiga chenga kipa Iker Cassilas na kufunga akisaidiwa na Wesley Sneidjer .
23:37 Arjen Robben aipasua safu ya ulinzi ya Uhispania na kufunga bao la Tano la Uholanzi.
23:37 GOOOOOAL
23:31 Uholanzi 4-1 Uhispania dakika ya 71
23:23 Stefan de Vrij ndiye mfungaji wa bao hilo kutokana na Free kick.
23:31 Van Persie amwadhibu kipa Iker Cassillas na bao la 4 .
23:30 GOOOOOOAL!
23:32 Uholanzi wanajipatia bao la tatu kwa mkwaju wa kichwa
23:32 GOOOOOOOOOAL
23:31 Free kick kuelekea lango la Uhispania baada ya Pique kuunawa mpra.
23:21 Fernando Toorres na Pedro wanaingia kwa upande wa Uhispania kuziba pengo lililoachwa na Xavi Alonso na Diego Costa.
23:24 Van Persie aoneshwa kadi ya njano kwa kucheza visivyo
23:19 De Guzman anaondoka na kupumzishwana na pahala pake panachukuliwa na Georginio .
23:17 Uhispania imenusurika kichapo zaidi baada ya mkwaju wa Van Persie kuugonga chuma
23:12 Arjen Roben aiweka Uhoplanzi mbele baada ya kuwazunguka madefenda wawili na kumwacha kipa na nahodha wa Uhispania Iker Cassillas ameduwaa.
23:10 GOOOOOOAL . Uhispania 1-2 Uholanzi dakika ya 54.
23:08 Uholanzi inafanya mashambulizi katika lango la Uhispania lakini ukuta umewekwa kikamilifu.
23:03 Mabao bado ni Uhispania 1-1 Uholanzi dakika ni ya 46 ya kipindi cha pili .
23:02 Kipindi cha pili kinaanza katika uwanja wa Fonte Nova, ulioko Salvador Brazil
22:45 Uhispania 1-1 Uholanzi dakika ni ya 45
22:44 GOOOOOOAL Robin van Persi aiswazishia Uholanzi kunako dakika ya 44 ya kipindi cha kwanza kwa kichwa .
22:43 Zimesalia dakika mbili kipindi cha kwanza kikamilike mabao bado ni Uhispania 1-0 Uholanzi
22:41Offside Arjen Roben apatikana amejenga kibanda katika ardhi ya Uhispania baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Van Persie
22:38 Uhispania imedhibiti asili mia 68 ya mechi hii huku Uholanzi wakitawala asili mia 32 pekee ya mechi hii.
22:36 Offside, Daryl Janmaat anammegea Robin van Persie pasi safi lakini msaidizi wa refarii anas=inua kibendera na kusema alikuwa keshaotea .
27:30 Offside, Holland. Bruno Martins Indi tries a through ball, but Robin van Persie is caught offside.
22:32 Uhispania 1-0 Uholanzi
22:32 Uhispania inaongoza 1-0 Uholanzi.dakika ni ya 34 ya kipindi cha kwanza .
22:28 Wimbi lingine la shambulizi kutoka kwa Wahispania
22:27 GOOOOOOAL Xavi Alonso anaiweka Uhispania mbele baada ya Diego costa kuangushwa .
22:27 Xavi alonso ndiye anayeupiga.
22:26 Penalti kwa Uhispania .
22:25 Kadi ya Njano Guzmanamwangusha Iniesta
22:22 Kona kuelekea upande wa Uholanzi lakini Ramos anakosa kuitumia kikamilifu na inakuwa ni Goal Kick !
22:20 Shambulizi la UHispania likiongozwa na Diego Costaakisaidiwa na David Silva latibuka .
22:02 Uhispania inaanza kuonesha keke zake katika mechi hii iliyosheheni nyota wa Manchester United Robin van Persie Nahodha wa Real Madrid Iker Cassillas Cesc Fabregas Xavi Alonso Gerrad Pique Arjen Robben miongoni mwa wengine wengi.
22:02 Hiyo ndiyo iliyokuwa fainali ya tatu kwa Uholanzi bila ya mafanikio.
22:01 Timu hizi sio geni katika mechi zenye hadhi kama hii, Uhispania iliilaza Uholanza katika fainali huo Afrik kusini kabla ya kutawazwa mabingwa wa dunia.
22:01
22:00 Mechi ya marudio ya fainali ya kombe la dunia la mwaka wa 2010 inaanza wakati wowowte kutokea sasa huko Salvador Brazil katika uwanja wa Fonte Nova .