Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiambatana na ujumbe wa Tanzania kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika Mjini Malabo, Equatorial Guinea. Miongoni mwa masuala muhimu yanayotarajiwa kujadiliwa kwenye mkutano huu ni bajeti ya umoja huo na mkakati wa kukusanya maoni kutoka nchi wanachama kuhusu Afrika ifikapo mwaka 2063, ambapo umajo huu utafikisha miaka mia moja.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wajumbe wenzake wa kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika unaofanyika Mjini Malabo, Equatorial Guinea.
Viongozi wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika wakiwa kwenye picha ya Pamoja.Picha na IKULU.