Dairekta wa filamu ya Half of a Yellow Sun, Biyi Bandele akizungumza na wadau wa sinema kabla sinema yake hajafanyiwa Primia ya Afrika mjini Zanzibar. Kushoto ni mratibu wa majaji ZIFF, Fabrizio Colombo kutoka Italia.
Na Mwandishi wetu, Zanzibar
TANZANIA imebahatika kufanya Primia ya Afrika kwa sinema ya Half of a Yellow Sun , miezi miwili tu baada ya sinema hiyo kuzuiwa kimtindo nchini Nigeria ambako mtengenezaji ndiko nyumbani kwake.
Sinema hiyo ilioneshwa jana katika ukumbi wa wazi wa Ngome Kongwe.
Sinema hiyo ambayo imefanyiwa kazi kwa miaka 6 ni miongoni mwa sinema ndefu bora tatu ambazo zipo katika mashindano kwenye tamasha la filamu la Kimataifa la Zanzibar, ZIFF.
Sinema nyingine zenye ubora mkubwa na ambazo zimevutia wapenzi wengi wa sinema ni The Thorn of The Rose kutoka Guinea Bissau na Mandela:Long walk to Freedom ya Afrika Kusini.
Pamoja na ugumu wa masuala mbalimbali yanayozungumzwa katika filamu za The Thorn of The Rose na Half of a Yellow Sun watu wa Zanzibar wakiwemo madairekta, maprojuza na waigizaji wa ngazi za kimataifa 30 kutoka nchi 14 mbalimbali walizikubali filamu hizo.
Filamu iliyoleta kizaazaa kikubwa cha fikira ni The Thorn of the Rose. Sinema hii ya aksheni yenye mapenzi yenye vurugu, rushwa , utendaji mbovu wa wanasiasa na vyombo vya dola na imani kuhusu mzimu uliofanyiwa vibaya ukiwa dunia kutopumzika mpaka mambo yamerekebishwa si ajabu ikatwaa tuzo kwa jinsi ilivyotulia.
Muigizaji wa sinema hii Ady de Batista kutoka Guinnea Bassau alikuwepo kushuhudia namna ambavyo wapenzi wa sinema wanavyoipokea sinema yake hiyo yenye ukakasi maeneo mengine, hasa ubakaji uliokuwa unafanywa na ofisa wa polisi cha mdada mhusika hadi kifo chake.
Wasanii mbalimbali na waandishi wa habari wakiwa katika moja ya mikutano ya wasanii na waandishi wa habari kwenye tamasha linaloendelea la nchi za majahazi ZIFF mjini Zanzibar.(Picha zote na zainul Mzige wa Mo blog).
Sinema ya Half of a Yellow Sun, inayotambulika kimataifa na kufanya vyema katika mabara mengine, ilkioneshwa kwa mara ya kwanza katika bara la Afrika nchini Tanzania katika onesho la Jumatano wiki hii Ngome Kongwe.
Sinema hiyo iliyotokana na kitabu chenye jina kama hilo cha mwaka 2006 iliyoandikwa na kuongozwa na Biyi Bandele inaonesha namna gani dairekta huyo amekomaa katika miaka yake 20 ya utengenezaji wa sinema.
Sinema hiyo ambayo ilizuiwa kuoneshwa Nigeria miezi miwili iliyopita katika kile ilichodai bodi ya sensa ya nchi huyo kutoona mahali sinema hiyo inaweza kufiti katika viwango cha uonekanaji na dai la kuwa inaweza kuchochea ghasia, ni moja ya sinema iliyoangalia kwa undani vurugu za Biafra na maisha kuendelea ndani ya vurugu hizo.
Ikiwa imetumia miaka sita kutengenezwa sinema hiyo ni moja ya sinema tunazoweza kusema kwamba ni babu kubwa kutokana na simulizi lake na uigizaji ukiongozwa na kinara wake Thandie Newton.
Pamoja na kwamba Bandele amekuwa akilaumiwa kwa kumweka Newton katika kinara cha uigizaji katika simulizi hilo anasema kwamba hiyo si kweli kwani anaona kwamba kazi na maamuzi yake yamekuwa mema na ya maana zaidi kuliko kipindi chochote cha kazi yake kama dairekta.
Pamoja na kuonesha sinema tamasha la 17 la filamu la ZIFF pia limeendelea na program zake nyingine kama watoto na wanawake na soko la wanawake mwaka huu limefanya vyema zaidi.