Friday, June 20, 2014

MARUFUKU POLISI JAMII KUTUMIA SILAHA



MARUFUKU POLISI JAMII KUTUMIA SILAHA
KAMISHNA wa Polisi Jamii nchini, Musa Ally Musa, amepiga marufuku Polisi Jamii kutumia silaha za mapanga katika ulinzi badala yake watumie filimbi.
Musa alitoa agizo hilo jijini Dar es Salaam jana, alipozungumza na waandishi wa habari na kusema kutokana na changamoto iliyopo kwa jamii, ya kutokuelewa maana ya Polisi Jamii kunachangia polisi hao kuonekana kama majambazi.
Alisema Polisi Jamii wanapoona tukio la uhalifu wanatakiwa watumie filimbi kwa kuwa wengi wao hawana sare wala vitambulisho, pia watoe taarifa kwa askari kata ambaye yupo  eneo la tukio ambaye ndiye mwenye majukumu ya kutoa silaha.
 Tangu kuanzishwa kwa Polisi Jamii mwaka 2006, imesaidia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa vitendo vya uhalifu
alisema.
Alisema Polisi Jamii maana yake ni ushirikishwaji wa kila mtu aliyemo ndani ya Jamii kulingana na nafasi yake aliyokuwa nayo.