Kitu cha pili kambani: Ivan Perisic (wa pili kulia)akipongezwa na wenzake baada ya kufunga bao la pili.
KITENDO cha Alex Song kumfanyia madhambi mshambuliaji wa Croatia, Mario Mandzukic na kuoneshwa kadi nyekundu rasmi kimeua matumaini ya Cameroon kufuzu hatua ya 16 ya kombe la dunia katika kundi A mjini mjini Manaus.
Song alishikwa na hasira dakika ya 40 na kufanya kitendo cha kinyama kwa Mandzukic wakati huo Cameroon ikiwa nyuma kwa bao 1-0.
Baada ya Hispania kutupwa nje ya michuano, Cameroon imekuwa nchi ya kwanza kwa Afrika kufangasha virago katika fainali za kombe la dunia mwaka huu kutokana na kipigo kikubwa cha mabao 4-0 dhidi ya Croatia.
Kufuatia kadi nyekundu ya Song, mambo yalikwenda kombo zaidi na kushuhudia Cameroon wakimalizia usiku vibaya baada ya kufungwa mabao matatu kipindi cha pili na ndoto za kufuzu kuzimwa kabisa.
Hata hivyo kituko kikubwa ni beki wa Tottenham Benoit Assou-Ekotto kuamua kupigana na mwenzake Benjamin Moukandjo katika hatua za mwisho za mchezo huo.
Hapa chini ni vikosi vya wachezaji na viwango vyao. Alama zimetolewa chini ya 10
Kikosi cha Cameroon: Itanjde 4.5; Mbia 4, Chedjou 4.5 (Nounkeu 46, 3), N'Koulou 4.5, Assou-Ekotto 5; Song 2, Matip 5, Enoh 5; Moukandjo 4, Aboubakar 7 (Webo 70, 7), Choupo 6 (Salli 5).
Wachezaji wa akiba ambao hawakucheza: Feudjou, Djeugoue, N'Guemo, Eto'o, Makoun, Bedimo, Fabrice, Nyom, N'Djock.
Kadi nyekundu: Song.
Kikosi cha Croatia: Croatia: Pletikosa 6; Srna 7.5, Lovren 6, Corluka 6, Pranjic 7; Rakitic 7.5, Modric 7.5, Sammir 6.5 (Kovacic 70, 7); Perisic 8.5 (Rebic 78, 6), Mandzukic 7, Olic 8 (Eduardo 69, 7).
Wachezaji wa akiba ambao hawakucheza: Zelenika, Vrsaljko, Vukojevic, Jelavic, Schildenfeld, Brozovic, Mocinic, Vida, Subasic.
Kadi ya njano: Eduardo.
Waliofunga magoli: Olic 11, Perisic 48, Mandzukic 61, 73
Idadi ya watazamaji: 36,000
Mwamuzi: Pedro Proenca (Portugal)
Mchezaji bora wa mechi: Ivan Perisic
Kijana nakutua chini!: Danijel Pranjic akichuano vikali na Benjamin Moukandjo dakika za mwanzo za mechi.
Mashabiki wa Croati wakiishangilia timu yao ya taifa.
Huyu jamaa aliishangilia sana Cameroon, lakini akaishia kulia tu.
Acha zako mwanangu!: Assou-Ekotto na Moukandjo walipigana baada ya kipigo hicho.