Friday, June 27, 2014

ALIYETIWA MENO NA LUIS SUAREZ AFUNGUKA `MAZITO YA MOYONI`



ALIYETIWA MENO NA LUIS SUAREZ AFUNGUKA `MAZITO YA MOYONI`
All smiles: Giorgio                  Chiellini feels no malice towards Luis Suarez after his                  bite
Tabasamu kubwa: Giorgio Chiellini ameumia na adhabu aliyopewa Suarez kwa kung`ata yeye.

Imechapishwa Juni 27, 2014, saa 9:20 alasiri

BEKI wa Italia, Giorgio Chiellini amefunguka kutokana na adhabu aliyopewa  Luis Suarez kwa kumng`ata.
 Suarez amefungiwa na FIFA  mechi tisa za kimataifa za Uruguay na miezi minne ya kutocheza soka.
Mshambuliaji huyo wa Liverpool aling`ata kwa mara ya tatu katika maisha yake ya soka baada ya kumshambulia Chiellini wa Italia na kumtia meno katika dakika ya 80 ya mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi na kushuhudia Uruguay ikishinda kwa bao 1-0.
Looking glum: Suarez was                    banned from all football for four months after biting                    Chiellini
Suarez amefungia miezi minne kutocheza soka baada ya kumtia meno  Chiellini


Lakini kwa Italia kuwa nje ya mashindano,  Chiellini anaamini adhabu ya Suarez ni kali sana , hivyo anampa pole.
"Moyoni mwangu sina hisia za furaha, kisasi wala hasira dhidi ya Suarez kutokana na tukio lile lililotokea uwanjani na yamekwisha". Aliposti katika  mtandao wake rasmi.
"Hasira zangu kwasasa zimebaki kwenye mechi na matokeo. Ni wakati ambao namuwazia Suarez pekee na familia yake kwasababu watakuwa kwenye wakati mgumu sana".
"Nimeingia kwenye matatizo na wachezaji wakubwa, lakini naamini adhabu aliyopewa ni kubwa sana". 


Mouthful: Uruguay's Suarez was                caught (left) biting Italy's Giorgio Chiellini (right) in                Tuesday's clash
Hapa kitu cha meno tu: Suarez (kushoto) alinaswa na Kamera akimng`ata beki wa Italia Giorgio Chiellini (kulia) kwenye mechi ya jumanne.
Painful: Chiellini pulled                  down his shirt to show his marks from Suarez during                  their Group D match in Natal
Maumivu: Chiellini akivua jezi yake kuonesha sehemu aliyong`atwa na  Suarez wakati wa mechi yao ya kundi D mjini Natal.