Wednesday, May 28, 2014

Walemavu watatu Ruangwa wakabidhiwa pikipiki aina ya bajaji toka kwa JK



walemavu watatu Ruangwa wakabidhiwa pikipiki aina ya bajaji toka kwa JK
Na Abdulaziz Video, Ruangwa 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekabidhi pikipiki aina ya bajaj kwa walemavu watatu katika shughuli fupi iliyofanyika katika Kata ya Mandawa wilayani Ruangwa mkoani Lindi
 Shughuli ya makabidhiano inatimiza ahadi ambayo Mheshimiwa Rais aliitoa kwa walemavu hao watatu ili kufuatia ahadi aliyooitoa Mwishoni mwa mwaka jana alipokutana nao alipokuwa katika ziara yake mkoani humo kukagua shughuli za maendeleo.
  Akizungumza mara baada ya kukabidhi pikipiki hiyo kwa Niaba ya Rais Kikwete Naibu waziri wa Tamisemi Elimu ambae pia ni Mbunge wa Jimbo hilo Kassim Majaliwa amewaambia walemavu hao kuwa Rais Kikwete amefurahi sana kutimiza ahadi hiyo ili kusaidia kuchangia uchumi wa walemavu hao ili wajiongezee kipato chao 
Aidha Majaliwa aliwaagiza Viongozi wa kata na kijiji kutoa usaidizi wa kutunza na kusimamia matumizi ya bajaji hiyo ili Iweze kuwa salama na walemavu hao kunufaika na msaada wa Rais Kwa Upande Katibu Tawala wilaya ya Ruangwa ,Silvanus Kilowoko alieleza kuhusiana na Msaada huo alieleza kuwa ofisi yake ilipokea fedha za kununulia bajaj hiyo na tayari wamefanikisha kuisajiri kabla ya kukabidhiwa kwa walengwa 
Akitoa shukrani kwa Niaba ya Ya walemavu hao ambao ni Saidi Kunamba.Bakari Ndambile na Bi Nassim Ramadhan , Mwenyekiti wa CCM Wilayani humo Bw Issa Njinjo kwa upande wake alisisitiza juu ya matumizi ya bajaj hiyo ikiwemo kujiongezea kipato
Naibu waziri wa Tamisemi Elimu ambae pia ni Mbunge wa Jimbo hilo Kassim Majaliwa akikabidhi Bajaji hizo kwa walengwa
Naibu waziri wa Tamisemi Elimu ambae pia ni Mbunge wa Jimbo hilo Kassim Majaliwa akimkabidhi Bi Nassim Ramadhan Bajaji yake
Wananchi wakishuhudia makabidhiano hayo
walemavu waliokabidhiwa Bajaji  Saidi Kunamba.Bakari Ndambile na Bi Nassim Ramadhan wakifurahia zawadi hizo