![]() |
| Muimbaji injili maarufu Tanzania Flora Mbasha akiwa na mumewe Emmanuel Mbasha, ambaye anatafutwa na polisi kwa tuhuma za kumbaka shemeji yake mwenye umri wa miaka 17. |
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Ilala jijini Dar Es Salaam linamsaka kwa udi na
uvumba Emmanuel Mbasha (pichani) ambaye ni mume wa mwimbaji maarufu wa
nyimbo za injili nchini, Flora Mbasha kwa madai ya kumbaka shemeji yake
mwenye miaka 17 (jina tunalo) ambaye ni yatima.
Taarifa
zilizopatikana ndani ya jeshi hilo kupitia vyanzo vyetu makini zinadai
kwamba mlalamikaji huyo alifika kituoni hapo Jumatatu iliyopita muda
wa mchana na kufungua kesi yenye Kumbukumbu Na. TBT/RB/3191/2014 na ya
Jalada la Uchunguzi Na. TBT/IR/1865/2014 akidai kufanyiwa unyama huo
kwa siku mbili (Ijumaa na Jumapili) wiki iliyopita nyumbani kwa Mbasha,
Tabata-Kimanga, Dar Es Salaam.
Ilidaiwa
kuwa, Ijumaa iliyopita mlalamikiwa alifanya kitendo hicho sebuleni
nyumbani na Jumapili ilidaiwa alitekeleza ukatili wake huo ndani ya
gari lake hali ambayo ilimfanya mlalamikaji kutoa taarifa Kituo cha
Polisi, Tabara-Aroma jijini Dar Es Salaam.
Iliendelea
kudaiwa kuwa, kufuatia maumivu makali aliyoyapata mlalamikaji huyo
ilibidi aende Hospitali ya Amana na kugundulika kuwa aliingiliwa
kimapenzi na kumsababishia michubuko sehemu za siri.
HISTORIA YA MLALAMIKAJI
Mlalamikaji ni kati ya watoto mapacha waliozaliwa jijini Mwanza na mama ambaye jina lake halikupatikana mara moja.
Mama
wa mtoto huyo (kwa sasa ni marehemu pamoja na mume wake) akiwa muumini
wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God (EAGT) aliamua kumtoa mtoto
mmoja kwa mama mzazi wa Flora Mbasha kwa lengo la kumlea, wakati huo
mtoto huyo alikuwa na miezi mitatu.
Ikaelezwa
kuwa, mama wa Flora alikaa na mtoto huyo akimsomesha hadi alipofika
darasa la saba ambapo alimkabidhi kwa Flora na kuishi naye hadi
alipofikwa na janga hilo.
Maelezo
zaidi yanasema Mbasha aliweza kufanya kitendo hicho kwa sababu mkewe
(Flora) ameondoka nyumbani na kwenda kuishi hotelini kwa kile
kilichodaiwa kwamba kuna ugomvi mkubwa ndani ya ndoa yao.
Taarifa
zaidi zinadai kwa sasa Mbasha naye hayupo nyumbani kwake huku
mlalamikaji yuko Hospitali ya Amana akiendelea kufanyiwa uchunguzi wa
kiafya ili kubaini kama ana maambukizi ya magonjwa ya zinaa au la!
Kwa
upande wake mlalamikaji huyo alipopigiwa simu juzi kwa lengo la
kuthibitisha kuhusiana na sakata hilo alikiri na kusema amekwishatoa
taarifa polisi kwa kitendo alichofanyiwa na mwenye nyumba huyo.
Chanzo: Global Publishers
