Friday, May 30, 2014

KINANA AKERWA NA UPORAJI WA MAENEO YA WANANCHI KUTOKA KWA BAADHI YA VIONGOZI WA CHAMA NA SERIKALI WILAYANI BABATI VIJIJINI




KINANA AKERWA NA UPORAJI WA MAENEO YA WANANCHI KUTOKA KWA BAADHI YA VIONGOZI WA CHAMA NA SERIKALI WILAYANI BABATI VIJIJINI
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akisikiliza maswali na changamoto mbalimbali walizonazo  kutoka kwa Wananchi wa kata ya Ayamango (Gallapo),Wilayani Babati Vijijini mkoani Manyara kwenye mkutano wa hadhara.Baada ya kusikiliza maswali kinana alionekana kukerwa kwa kiasi kikubwa wananchi wanavyoporwa maeneo yao na viongozi wa chama na Serikali wakiwemo na baadhi ya wawekezaji, Kinana aliahidi suala hilo ambalo limekithiri kwa kiasi kikubwa wilayani humo,kulitafutia ufumbuzi kwa kulipeleka katika vikao vya juu vya chama hicho.

 Kinana alisikitishwa zaidi  kwa namna ambavyo wananchi vijijini wanavyoporwa ardhi na  baadhi ya viongozi wa chama na serikali wakiwemo na baadhi ya wawekezaji,huku wakitumia mahakama kuchelewesha haki zao,Kinana amesema kuwa viongozi wasiotimiza wajibu wao Mkoa wa Manyara atawaburuza kwa Rais.

Kinana ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi,siasa na Uenezi Nape Nnauye,wakiwa kwenye ziara ya siku saba ya kukagua kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Chama,kukagua maandalizi ya uchaguzi ya serikali za mitaa,kusikiliza kero za wananchi na kuzitafututia ufumbuzi.
 Baadhi ya Wanahabari walioko kwenye msafara wa Katibu Mkuu,Ndugu Kinana wakiwa kazini.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipokelewa na Wananchi wa kata ya Ayamango (Gallapo),Wilayani Babati Vijijini mkoani Manyara alipokwenda kuzindua shina la Wakereketwa,kutoa kadi kwa wanachama wapya sambamba na kufanya mkutano wa hadhara.
 Wananchi wa kata ya Ayamango (Gallapo),Wilayani Babati Vijijini mkoani Manyara wakimpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokwenda kuzindua shina la Wakereketwa,kutoa kadi kwa wanachama wapya sambamba na kufanya mkutano wa hadhara.
 Wananchi wa kata ya Ayamango na mabango yao.
 Wakifuatilia mkutano wa hadhara katika kata ya Ayamongo,Babati Vijijini mkoani Manyara
 Katibu wa NEC Itikadi,Sisa na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye akiwahutubia  Wananchi wa kata ya Ayamango (Gallapo),Wilayani Babati Vijijini mkoani Manyara alipokwenda kuzindua shina la Wakereketwa,kutoa kadi kwa wanachama wapya sambamba na kufanya mkutano wa hadhara.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameongozana na Mbunge wa jimbo la Babati Vijijini,Mh.Jitu Son na viongozi mbalimbali wachama wa Wilaya na Mkoa,wakikagua moja ya jengo la mradi wa ujenzi wa chuo cha Ualimu cha Sayansi Mamire,wilayani Babati vijijini mkoani Manyara.

PICHA NA MICHUZIJR-BABATI VIJIJINI- MANYARA.