Monday, May 12, 2014

DEREVA BODABODA ACHINJWA-KISARAWE II KIGAMBONI

 
 
 


Bi. Sakina, ambaye ni mama mzazi wa John Thobias akiweka shada la maua kwa uchungu.
Katekista Millinga akiweka msalaba.
Jeneza likiwa ndani ya kaburi.
Mwili wa marehemu ukipelekwa makaburi ya Magogoni-Kigamboni.
 Hizi ni pikipiki za vijana wa bodaboda zikiwa zimepaki jirani na msibani.
  Bodaboda wakijipanga toka nyumbani mpaka makaburini kwa ajili ya kuubeba mwili wa marehemu.
Bodaboda huyu alizuiwa kwa muda ili kwenda kuzika mwili wa mwenzao.
Bw. Joseph mjomba wa marehemu akiwa karibu na jeneza.
 John enzi za uhai wake.
Familia ya marehemu John ikiwa pamoja baada ya mazishi.
  Hiki ndicho kibanda kilichoandaliwa kwa ajili ya kufanyia tambiko ya mila kwa mwili wa John kabla ya kuagwa na kuzikwa.
MJI wa Kigamboni umegubikwa na majonzi mazito na vilio kutawala kila kona kufuatia kijana aliyefahamika kwa jina la John Thobias Joseph (19), dereva wa bodaboda maeneo ya Magogoni Kigamboni, kuchinjwa kisha pikipiki yake kuchukuliwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi.
Inasemekana John, alipigiwa simu na mtu asiyemfahamu akimtaka akamchukue na kumpeleka Kisarawe II, baada ya maongezi, John alionekana kumfahamu mteja huyo na kumuahidi kumfuata.
Inasemekana John alikuwa amembeba mama yake mdogo wakitokea hospitali, ambapo alimshusha mama na kumfuata mteja huyo.
Akisimulia bodaboda mwenziye alisema "John huwa na taratibu za kufika kijiweni asubuhi (mtaa wa Tungi kwa Matenga ambapo anapaki) lakini siku ya tukio haikuwa hivyo, jambo lililowashangaza wenzake na mmoja wao akaamua kumpigia simu lakini iliita pasipo kupokelewa.
"Baada ya kumtafuta kwa muda bila mafanikio ndipo tukapata taarifa za kuwapo kijana mmoja aliyekutwa amekufa nje ya mji, ndipo tukaamua kwenda eneo la tukio na kumkuta ni John'' alisema kijana huyo.

Aidha Katekista Millinga, akizungumza katika misa ya kuaga mwili wa marehemu huyo alisema, "Pengine wauaji wako hapahapa tulipo, sidhani kama wauaji wanatoka mbali, lakini maandiko yanasema, anayeuwa kwa upanga naye atauwawa kwa upanga."
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Engelbert Kiondo amekiri kutokea kwa tukio hilo na kutaka familia na wanabodaboda wote kuwa wavumilivu wakati uchunguzi ukiendelea.
Aidha, amewataka vijana wa bodaboda kuwa makini na abiria wanaowakodi,wasivutike na pesa nyingi wanazoahidiwa.
John, ambaye alikuwa ni kijana mdogo sana kiumri na hata umbo, alikutwa na mauti siku ya Alhamisi tarehe 8/05/2014 majira ya saa 8 mchana eneo la Kisarawe II, nje kidogo na Kigamboni.
Marehemu alizikwa jana tarehe 10/05/2014 katika  makaburi ya Magogoni-Kigamboni, Dar.
HAKIKA BWANA AMETOA NA SASA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.