Thursday, November 15, 2012

PICHA ZA MUSOMA MKOANI MARA.



 Kutokana na Ziwa Victoria kuwa na visiwa vingi usafiri wa aina hii hutumika zaidi kusafirisha abiria, kituko kwenye usafiri huo ni kwamba unafungwa mziki hata ikiwa umbali wa mita miatatu kutoka ufukweni unausikia baada ya kufungwa vipaza sauti vinavyotumika sana misikitini.
 Mmoja wa kina mama wa Musoma akiwa kazini na mkokoteni wake, kina mama wengi wa wilaya hiyo wamekua wakijishughulisha na kazi mbalimbali ambazo kwenye jamii nyengine zinaonekana kama kazi za wanaume pekee.
 Kando ya barabara kuu ya kuingia Musoma Mjini karibu na Stendi ya mabasi ya zamani.
 Eneo la kupandia kivuko cha MV Musoma kuelekea maeneo ya Kilese Tarime likiwa halina kizuizi chochote cha magari, ambapo ni hatari kwa usalama wa watu na magari yanayoelekea kwenye sehemu hiyo.
Mitaa ya Musoma Mjini.