TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, leo imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Harambee Stars, ya Kenya katika mchezo wa kirafiki wa Kimataifa uliomalizika hivi punde katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Bao la Stars, limefungwa katika dakika ya 5 na sekunde kadhaa kipindi cha kwanza na Aggrey Morris, na kufanya timu hizo zikienda mapumziko Stars ikiwa mbele matokeo yaliyodumu hadi kumalizika kwa mchezo huo.