Wednesday, October 10, 2012

SHABIKI WA YANGA AFARIKI BAADA YA KUSHINDA KWENYE SHINDANO LA KULA MENDE MAREKANI


 

Edward akila mende
Mshindi wa shindano la kula mende amefariki dunia muda mfupi kula mende wazima huko Florida -Marekani, polisi wamesema.

Edward Archbold, 32, ambaye alisema kwamba ameshawahi kula wadudu hao huko nyumbani kwao Dar es Salaam, Tanzania alianza kuumwa na hatimaye kuanguka katika duka la wadudu mahala ambapo shindano hilo lilikuwa likifanyika katika mji wa Deerfield Beach Ijumaa iliyopita.

Kuna zaidi ya watu 30 walioshiriki shindano hilo katika duka la Ben Siegel Reptile Store.
Mamalka zinasubiri matokeo ya vipimo vya hosptali ili kujua chanzo cha kifo cha Archbold.

Hakuna mtu yoyote aliyeshiriki kwenye shindano hilo aliyeumwa baada ya kumalizika kwa shindano hilo, walisema polisi.
"Tumesikitika sana juu ya tukio hili," alisema Ben Siegel , mmiliki wa duka la wadudu.
""Alionekana kama alitaka kujionyesha na alikuwa mtu mzuri sana," alisema, akiongeza kwamba Archbold hakuonekana kuwa anaumwa kabisa.

Mwanasheria wa Mr.Siegel alisema kwamba washiriki wote walisaini maelezo kwamba "wanakubaliana na matokeo yoyote yatakayotokea kutokana na kushiriki mchezo huo wa ajabu.

Mr.Archbold ambaye alikuwa anajulikana kwa mapenzi yake makubwa kwa timu ya Young Africans ya nchini Tanzania, alishinda shindano hilo lakini badae kidogo akadondoka na kufa.