Wednesday, October 03, 2012

MRADI WA AFYA YA UZAZI WAPATA MFADHILI MWENGINE. from MTAA KWA MTAA



Profesa wa Taasisi ya Kimataifa ya masuala ya Afya ya Karolinska Institutet  Chini ya taasisi ya World Lung Foundations Staffan Bergstrom M.D., Ph.D, akionyesha kiwango cha ongezeko la huduma za afya kwa mama wajawaziti na punguzo la idadi ya vifo, mbele ya waandishi wa habari wakati wa kutangaza kupatikana kwa mfadhili mwengine wa mradi wa huo jijini Dar es Salaam leo ambao unalengo la kupunguza vifo vya kina mama wajawazito. Awali ufadhili wa mradi huo ulikua unatolewa na Bloomberg Philanthropies kwa kushirikiana na Wizara ya afya lakini mfadhili mpya H&B Agerup Foundation ambae amesaini mkataba jana Jijini Newyork na kushuhudiwa na Rais Kikwete Ban Ki Moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ambapo inakadiriwa zaidi ya kinamama 50,000 hadi 2016 watafaidika.
Mganga Mfawidhi wa kituo Cha Afya Kibiti akieleza mbele ya waandishi wa habari namna mradi huo ulivyokua na mafanikio kwenye eneo hilo, ambapo amedai umesababisha hata baadhi ya watu wanaoshi jijini Dar es Salaam kufuata huduma zao kutokana na mafanikio ya mradi huo. Mradi huu ni wa maeneo yote muhimu kwa Afya ya mama mjamzito kuanzia vifaa wataalamu na hata miundombinu ya Hospitali.
Naibu Mkurugenzi wa Mradi ambaye ni Daktari bingwa wa upasuaji Dk. Hemed Mahfudh akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwa wandishi wa habari mara baada ya mkutano.