Sunday, October 07, 2012

Masalia ya mwili wa aliyekuwa Kardinali wa kwanza Mwafrika Mwadhama Laurian Rugambwa, yamezikwa rasmi katika Kanisa Kuu Jimbo Katoliki mjini Bukoba



Masalia  ya mwili wa aliyekuwa Kardinali wa kwanza Mwafrika Mwadhama Laurian Rugambwa, ambaye awali alizikwa kwenye Kanisa Katoliki la kwanza lililopo Kashozi mwaka 1997, mkoani Kagera, leo octoba 6 mwaka huu yamezikwa rasmi katika Kanisa Kuu Jimbo Katoliki mjini Bukoba, baada ya ukarabati wake kukamilika.


Aidha   mazishi hayo yameambatana na kumbukumbu ya miaka 100 ya kuzaliwa kwake.
Kardinali Rugambwa alizaliwa Julai 12,1912 ambapo mazishi hayo ni kumbukumbu muhimu kwa Watanzania na Waafrika kwa ujumla.
Historia ya Kardinali Rugambwa, alipewa Upadre mwaka 1943,  Uaskofu 1952, Ukardinali mwaka 1960 ambapo mwaka 1969 akawa Askofu Mkuu Jimbo la Dar es Salaam hadi alipostaafu mwaka 1992.
Kardinali Rugambwa alianzisha Kanisa Kuu Jimbo la Bukoba, kuleta Seminari Kuu ya Ntungamo na kujenga Shule ya Sekondari Rugambwa.
Pia alifanikisha ujenzi wa Hospitali ya Mugana, kuanzisha VIKOBA kwenye Parokia, Seminari Ndogo ya Visiga na Seminari Kuu ya Segerea iliyoko Dar es Salaam.

Kardinali Rugambwa alifariki Desemba 1997  ambapo Kardinali Rugambwa alizaliwa Kijiji cha Bukongo, Parokia ya Rutabo, Kata ya Kamachunu, Wilaya ya Muleba, mkoani Kagera akitokea katika familia iliyotukuka ya kitawala.
Alipata elimu ya Sekondari katika Shule ya Seminari Rubya Junior na kujiunga katika Semiri Kuu ya Katigondo, nchini Uganda, ambako alihitimu masomo ya Falsafa na Theolojia, Desemba 12, 1943