Monday, October 08, 2012

Mary Mwanjelwa ashindwa kutetea nafasi yake ya ujumbe wa Baraza Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM mkoa Mbeya



Mjumbe wa Baraza Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM mkoa, aliyekuwa akitetea nafasi hiyo Dk.Mary alijikuta akishindwa vibaya na mpinzani wake mkubwa kisiasa, Edina Mwaigomole.

Dk.Mary na Edina ni wanasiasa wanaokubalika ndani ya UWT mkoani hapa na wenye upinzani mkali kisiasa, kwani hata katika kinyang’anyiro cha ubunge viti maalum mkoani hapa walishindana kwa kura chache.

Nafasi ya ujumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa, ambayo ilikuwa na wagombea watatu, Shizya Mwakatundu, ambaye pia ni Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Mbeya mjini ameibuka kidedea.

Nafasi ya Mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM mkoa ilichukuliwa na Jane Dussu, wakati nafasi ya Uwakilishi wa Jumuia ya Wazazi ilinyakuliwa na Florence Mwakanyamale huku, Uwakilishi wa Vijana ukichukuliwa na Maryprisca Mahundi.