Warembo walioingi kwenye hatua ya tano Bora ya Redd's Miss Photo Genic.toka kulia ni Magdalena Roy (Mshiriki namba 6,kutoka Dar City Center - Kanda ya Ilala),Babylove Kalala (Mshiriki namba 9, kutoka Kagera - Kanda ya Ziwa), Lightness Michael (Mshiriki namba 5,kutoka Dodoma - Kanda ya Kati),Lucy Stephano (Mshiriki namba 4, kutoka Manyara - Kanda ya Kaskazini) na Diana Hussein (Mshiriki namba 20 ,kutoka Dar Indian Ocean - Kanda ya Kinondoni, Dar es Salaam.)
Mshiriki namba 4,kutoka Manyara - Kanda ya Kaskazini,Lucy Stephano ndie alieweza kuibuka kinara wa Kinyang'anyiro cha Redd's Miss Photo Genic 2012.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Rino Agency na Muandaani Mkuu wa Mashindano ya Miss Tanzanzia,Hashim Lundega akitangaza Mshindi wa Redd's Miss Photo Genic ambaye ni Mshiriki kutoka Manyara - Kanda ya Kaskazini,Lucy Stephano (katikati).hafla ya shindano hilo ilifanyika jana usiku kwenye Ukumbi wa hoteli ya E'Manyata Lodge,Monduli jijini Arusha.
Warembo walioingi kwenye hatua ya tano Bora ya Redd's Miss Photo Genic wakimshangilia mwenzao alieibuka mshindi wa Taji hilo mara baada ya kutangazwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Rino Agency na Muandaani Mkuu wa Mashindano ya Miss Tanzanzia,Hashim Lundega.
Warembo wenye vipaji vya kuimba wakitoa Burudani Mbele ya Warembo wenzao wa Redd's Miss Tanzania 2012.
Jaji Mkuu wa Shindano la Redd's Miss Photogenic 2012,Mroki Mroki asema maneno machache kabla ya kuanza kutangaza tano bora ya Warembo walioingia kwenye kinyang'anyiro hicho.
Mkuu wa Itifaki na Nidhamu ya Miss Tanzania, Albert Makoye akitoa muongozo kwa warembo hao.