Friday, October 05, 2012

KATIBU MWENEZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) WILAYA YA MBEYA MJINI AANZA MBWEMBWE




 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi(CCM) wilaya ya Mbeya Mjini ambaye pia ni Mkurugenzi wa kituo cha redio cha Sweet fm cha Jijini Mbeya Emmanuel Mbuza amekabidhi msaada kwa wafungwa wa Gereza la Ruanda wenye thamani ya zaidi ya shilingi Laki tano.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mbeya Mjini ambaye pia ni Mkurugenzi wa kituo cha redio cha Sweet Fm, Emmanuel Mbuza akisisitiza jambo kabla ya kwenda  kukabidhi msaada katika Gereza la Ruanda Jijini hapa.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mbeya Mjini ambaye pia ni Mkurugenzi wa kituo cha redio cha Sweet Fm, Emmanuel Mbuza akionesha baadhi ya vitu alivyokuwa anatarajia kuvitoa  katika Gereza la Ruanda Jijini hapa.


Na Emanuel Madafa,Mbeya
 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbeya Mjini ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Radio cha Sweet Fm iliyopo jijini hapa Ndugu Emanuel Mbuza ametoa msaada wa mahitaji mbalimbali katika Gereza la Ruanda .
 
Vitu vilivyo tolewa na Katibu huyo ni pamoja na Sabuni ,mafuta ya kupaka ,pedi ,miswaki,na dawa za meno ambavyo vyote vinagharimu ya zaidi ya  laki5.
 
Akikabidhi Msaada huo Mbuza amesema yeye binafsi na kama kiongozi wa chama anapaswa kuhudumia makundi yote bila kujali itikadi ya vyama wala dini hasa kwa kundi kama hilo la wafungwa ambao wanahitaji msaada mkubwa hasa kwa mahitaji muhimu kama hayo yaliyo tolewa.
 
Amesema nivema kila mmoja katika shughuki zake akajaribu kujiwekea utaratibu wa kutoa misaada kwa makundi mbalimbali  badala ya kuiachia jukumu hilo serikali pekee.
 
Kutokana na hali hiyo Mbuza amesema mara baada ya kupatiwa nafasi hiyo ya uongozi ndani ya chama cha mapinduzi ambacho ndicho chenye serikali atahakikisha anatumia fursa hiyo kuwatumikia wananchi wa Jiji la Mbeya kwa moyo wake wote kama alivyo ahidi wakati akiomba kupatiwa nafsi hiyo ndani ya Chama hicho cha CCM.
 
Aidha katika hatua nyingine Katibu huyo amewataka wananchi wa Jiji hilo kuendelea kukipa nguvu chama cha mapinduzi ili kiendelee kuwaletea wananchi wake maendeleo kwani katika kipindi hiki cha sasa asilimia kubwa ya viongozi wa chama ngazi ya Wilaya na Mkoa imeshikiliwa na vijana wenye nguvu na uwezo wa kuwatumikia wananchi wake.