Hali ya kingo katika bandari ya Malindi Mjini Zanzibar katika eneo la boti za uvuvi na majahazi lipo katika hali mbaya kutokana na kingo za bandari hiyo kubomoka na kuharibika kabisa jambo ambalo linaweza kuleta mmomonyoko wa udongo kama patatokea mawimbi makubwa ‘sunami’ katika bahari ya hindi. Ni vyema Mamlaka husika kuchukua hatua za haraka kulifanyia ukarabati eneo hilo.