Sunday, October 14, 2012

BREAKING NEWZ.MWEKA HAZINA IRINGA PRESS CLUB MWANAHABARI VICKY MACHA AFARIKI DUNIA GHAFLA




TAARIFA  kutoka mkoani Iringa ambazo zimeufikia mtandao  huu  wa www.francisgodwin.blogspot.com asubuhi  hii zinadai  kuwa aliyekuwa mweka hazina  wa chama cha  waandishi  wa habari  mkoa  wa Iringa(IPC) na mwandishi wa magazeti ya NIpashe mkoa  wa Iringa Vichky Macha (pichani) amefariki dunia asubuhi hii.


Vicky Macha kabla ya kifo chake alikuwa amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Iringa akisumbulia ugonjwa wa Maralia na kulazwa katika Hospitali ya mkoa  wa Iringa kabla ya leo asubuhi hii kufariki dunia.
Vicky Macha katika uhai  wake  alipata  kufanya kazi kwa karibu na marehemu Daudi Mwangosi ambaye alikuwa ni mwenyekiti wa (IPC) na hata siku  aliyefariki  dunia Vicky Macha kama mweka hazina wa IPC mara baada ya  kumweleza juu ya kifo cha Mwangosi alipoteza fahamu kwa muda katika ofisi za IPC .

Hata  hivyo kutokana na siku ya tukio viongozi mkuu nilikuwa ni mimi Francis Godwin ambaye nilikuwa ni naibu katibu mkuu  wa IPC  kwa  kushirikiana na vema na Vicky  tuliweza kujikaza  na kuhakikisha mambo yanakwenda  vema japo mara kwa mara mwenzake alikuwa akiishiwa nguvu na mimi pia nikiishiwa nguvu na kujikuta  tukibembelezana na kujikaza.


 Rais  wa umoja  wa vilabu  vya  waandishi  wa habari Tanzania (UTPC) Keneth Simbaya (kulia) akikabidhi mchango wa rambi rambi ya  kifo cha Mwangosi  kwa makamu mwenyekiti wa IPC Francis Godwin kutoka kwa vilabu mbali mbali vya wanabari nchini kwa ajili ya kifo hicho , katikati ni marehemu Vicky Macha akilia kwa uchungu  na kushoto ni katibu mtendaji wa IPC Frank Leonard.

Taarifa  zaidi  tutaendelea  kuwaletea hapa
jambo kwa  sasa naweza  kusema Bwana ametoa na Bwana ametwaa  jina lake na lihimidiwe milele