Sunday, September 23, 2012

YANGA 4 - 1 JKT - AZAM 1-0 MTIBWA



             Wachezaji wa Yanga, wakimpongeza Kavumbangu baada ya kufunga bao la pili

                                                  Cannavaro anafunga bao la kwanza
                                    Kiiza na Kavumbangu wakimpongeza Cannavaro


         Chuji akimuelekeza Niyonzima namna ya kupiga mpira wa adhabu uliozaa bao la kwanza 

                DUWA LA KUKU; Wachezaji wa JKT wakiomba dua kabla ya mechi

                                         Kavumbangu akishangilia bao la nne
    Mwenyekiti wa Yanga, akitoka kwenye chumba cha wachezaji wakati wa mapumziko

YANGA SC jioni hii imepata ushindi wa kwanza ndani ya mechi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuifunga JKT Ruvu mabao 4-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Hadi mapumziko Yanga walikuwa tayari mbele kwa mabao 2-0, yaliyotiwa kimiani na Nahodha, Nadir Haroub Ally ‘Cannavaro’ dakika ya nne na Didier Kavumbangu dakika ya 31, mabao yote yakitokana na kazi nzuri ya kiungo mshambuliaji Simon Msuva.
Bao la kwanza ulikuwa mpira wa adhabu uliopigwa na Haruna Niyonzima, baada ya Msuva kuangushwa karibu kabisa na eneo la hatari la JKT Ruvu na bao la pili dogo huyo aliyesajiliwa kutoka Moro United iliyoshuka daraja, alimpa pasi mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Kavumbangu.

Kipindi cha pili, Yanga walirudi tena kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la tatu dakika ya 52, mfungaji Simon Msuva kabla ya Didier Kavumbangu kufunga la nne dakika ya 65.
JKT ilipata bao lake la kufutia machozi dakika ya 68 mfungaji Credo Mwaipopo.
Katika mchezo wa leo, Yanga ilicheza vizuri, wachezaji wakionana kwa pasi nzuri ndefu na fupi, tofauti na ilivyokuwa kwenye iliyopita mjini Morogoro, ambako walifungwa 3-0 na Mtibwa Sugar.

Ikumbukwe mechi ya kwanza, Yanga ililazimishwa sare ya bila kufungana na Prisons mjini Mbeya.
Yanga leo ilicheza chini ya kocha Msaidizi, Freddy Felix Minziro, baada ya aliyekuwa Kocha Mkuu, Mbelgiji Tom Saintfiet kusitishiwa mkataba jana usiku, kufuatia kutofautiana na uongozi.