Wednesday, September 19, 2012

WAZIRI MKUU MHESHIMIWA MIZENGO PINDA AHITIMISHA ZIARA YAKE KATIKA MKOA WA MWANZA



 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda katikati, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Everest Ndikillo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Clement Mabina wakiwa na Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda wakati wa majumuisho ya ziara wa Waziri Mkuu katika Mikoa ya Mwanza, Geita na Shinyanga.

 
Mama Tunu Pinda akishuka kwenye gari ili aweze kuingia kwenye kikao cha majumuisho ya ziara ya Waziri Mkuu leo katika Halmshauri ya jiji la Mwanza.


 
Pinda akisalimiana na viongozi wa Mkoa wa Mwanza.

 
 Viongozi wa serikali kutoka Mikoa ya Geita, Shinyanga na Mwanza, Wadau na Waaandishi wa habari amabo wamejitokeza katika majumuisho hayo leo.

 
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Kondisaga akiwasilisha kwenye kusanyiko hilo.

 
Mawe matatu Kusanyikoni.....

 
Nukuu za Kusanyiko....

 
Kusanyiko.....

 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Afande Libearatus Ballow akiwa na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Wilson Mbonea Kabwe leo katika majumuisho ya ziara ya Waziri Mkuu.

 
Wakuu mbalimbali wa wilaya za miji kanda ya ziwa.

 
Waziri Mkuu akisalimiana na Mkurugenzi wa Moil Company Limited Mansoor Dogo mbele ya viongozi mbalimbali ya Serikali leo.

 

Waziri Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Kayanza Pinda amemeliza ziara yake leo katika mikoa ya Mwanza, Geita na Shinyanga kwa majumuisho yake ya mwisho yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya jiji la Mwanza.

Akiongea mbele ya viongozi mbalimbali wa serikali, vyama vya siasa, dini na waandishi wa habari, Pinda amesema kuwa amefurahishwa na ziara hiyo katika sehemu zote alizopita kwani kwake ilikuwa nidarasa kujionea fursa mbalimbali za maendeleo akisihi wananchi kuzitumia katika kujikwamua kutoka lindi la umasikini linalowakabili.

Pia amewaomba viongozi wa mikoa yote mitatu aliyozuru kuweka mpango mkakati wa kuibua fursa  zaidi za kimaendeleo ili kuwaletea Watanzania maisha bora.

Waziri huyo amemaliza ziara yake na kurejea jijini Dar es salaam jioni ya jana.