Friday, September 14, 2012

WATAALAM WAKUTANA RWANDA KUJADILI KUUNDWA KWA BENKI YA PAMOJA YA AFRIKA MASHARIKI.

 

Wataalam wenye thamana ya kushughulikia kuundwa kwa Benki ya Pamoja ya Nchi za Afrika Mashariki ameendelea tena na mkutano wao mjini Kigali kujadili mikakati ya uundwaji huo na taasisi nyingine katika ukanda huu.

Mchumi Mkuu wa Benki ya Taifa ya Rwanda anayeiwakilisha Rwanda katika majadiliano hayo Dkt. Frank Kigabo amesema katika mkutano huo mazungumzo yatalenga katika mada zilizobaki akiahidi kuwa hadi mwishoni mwa mkutano huo Jumamosi wiki hii ufumbuzi utapatikana.

Naye Katibu Mkuu Msaidizi anayeshughulikia Mipango na Miundombinu katika Sekretariet ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Enos Bukuku amesema wananchi wa Afrika mashariki wanasubiri kwa hamu kujua nini kutakachoamuliwa na mkutano huo.