Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (kushoto), akimkabidhi jagi, Godfrey Mpiuka aliyekuwa miongoni mwa washindi wa droo ndogo iliyofanyika nje ya stendi ya mabasi Ubungo, jijini Dar.
Mc Chaku Shemungia akiwa ameshika simu aina ya Galaxy aliyojishindia Koletha Mwanga kutoka Mbagala.
Meneja Masoko wa Global, Benjamini Mwanambuu (kushoto) akimkabidhi jagi la pili, Rehema Seneje.
Rehema Seneje aliyejishindia majagi mawili akielezea ambavyo amekuwa akijishindia zawadi mbalimbali katika bahati nasibu zinazoendeshwa na Global siri ya mafanikio ikiwa ni kusoma na kununua nakala nyingi za magazeti ya Global.
Abdallah Mrisho (kushoto) akimpatia T-shirt mmoja wa washindi.
Sehemu ya kuponi zilizoshindaniwa.
Mmoja wa wasomaji akichanganya kuponi ili kupata mshindi.
…akitaja mshindi. Pembeni yake ni MC Chaku.
Sehemu ya wakazi wa Dar wakifuatilia tukio hilo.
MC Chaku akisakata rhumba na mmoja wa wanenguaji.
Benjamini Mwanambuu (kushoto) akimkabidhi T-shirt, mshindi Agness Kasunga.
Agness Kasunga akiwa ndani ya T-shirt yake.
Mnenguaji, Latifah Charles na shabiki wakionyesha machejo wakati wa droo hiyo.
Wananchi wakijaza kuponi kabla ya droo kuanza.
Benjamini akimkabidhi Bakari Omunga wa Ubungo Bus Terminal T-shirt yake.
WAKAZI wa jiji la Dar es Salaam jana walipata fursa ya kushiriki droo ndogo ya shindano la Timiza Ndoto yako kwa kujishindia gari aina ya Toyota NOAH inayoendeshwa na kampuni ya Global Publishers Ltd wachapishaji wa magazeti ya Uwazi, Championi, Amani, Ijumaa na Risasi. Katika droo hiyo zawadi mbalimbali kama Jagi, T-shirt na Simu aina ya Galaxy zilitolewa. Shindano hili linaendelea mpaka Novemba itakapochezeshwa droo kubwa ambapo mshindi atajinyakulia NOAH. Akizungumza na mtandao huu, Meneja wa Global, Abdallah Mrisho alitoa wito kwa wananchi kote nchini kujipatia nakala za magazeti ya Global na kukata kuponi iliyo katika ukurasa wa pili wa kila gazeti ili waweze kujizolea zawadi mbalimbali zitakazokuwa zikitolewa na kampuni ya Global.
(PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS / GPL)