Friday, September 14, 2012

WANAFUNZI PAMOJA NA JAMII WAHAMASISHWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO.



 
Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Mradi wa ‘eSchools Connectivity’ nchini Tanzania Head of Cooperation wa Ubalozi wa Ufaransa hapa nchini Francois Leonard (wa pili kulia) akizindua chumba cha kompyuta katika Shule ya Sekondari ya Jangwani wakati wa uzinduzi wa mradi huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika Shule hiyo. Kushoto ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Kheri Kessy na kulia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Jangwani Margareth Doriye.
Uzinduzi wa chumba hicho umeashiria kuzinduliwa rasmi kwa mradi huo wa kuziunganisha shule na wanajamii wanazozizunguka kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
 
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Jangwani Margareth Doriye akitoa hotuba ya kumkaribisha mgeni rasmi pamoja na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa Mradi wa kuziunganisha shule kwa kutumia mtandao ‘e Schools Connectivity’ uliofanyika katika shule ya Jangwani jijini Dar es Salaam.
Mwl. Margareth Doriye pamoja na kutaja mafanikio pia amezungumzia changamoto zinazowakabili shuleni hapo ikiwa ni pamoja ongezeko la wanafunzi wenye ulemavu wa viungo ambalo haliendani na kupanuka kwa bweni na vifaa muhimu.
Aidha ametumia fursa hiyo kuwaomba wenye nia ya kusaidia wasisite kutoa msaada wao kwa vifaa muhimu kama vile viti vyenye magurudumu, magongo ya kutembelea na kuwa msaada wowote unakubalika.

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani wakifuatilia uzinduzi huo.
 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano Patrick Makungu akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kuzinduliwa kwa mradi wa ‘eSchools Connectivity’  ambapo pamoja na mambo mengine amesema katika hatua za kwanza tu mdari huo umeonyesha mafanikio na walengwa wameanza kupata mafanikio.
 
  Head of Cooperation wa Ubalozi wa Ufaransa hapa nchini Francois Leonard akielekezana na baadhi ya wanafunzi kuhusu matumizi ya teknolojia hiyo.
 
 Pichani juu na chini ni wanafunzi wa Sekondari ya Jangwani.
 
Wanafunzi hao wakiimba wimbo wa Shule. 
Wanafunzi hao wakiburudisha wageni kwa kucheza ngoma. 

Head of Cooperation wa Ubalozi wa Ufaransa hapa nchini Francois Leonard akiwa katika picha ya pamoja na walimu na wadau mbalimbali baada ya kuzindua Mradi wa Matimizi ya Teknolojia ya Habari miongoni mwa shule pamoja jamii.