Saturday, September 15, 2012

UBALOZI WA UJERUMANI NCHINI SUDAN NAO WAVAMIWA.



 
 Ubalozi wa Ujerumani nchini Sudan umevamiwa na waandamanaji wanaopinga filamu ya kumdhalilisha mtume Muhammad iliyotengenezwa nchini Marekani. 
Kundi la watu wenye hasira wapatao 5000 wamevamia ubalozi huo mjini Khartoum na kuushambulia.
Polisi wametumia mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji ambao pia waliulenga ubalozi wa Uingereza ulio jirani na wa Ujerumani.
Baadhi ya waandamanaji walifanikiwa kuingia ndani ya jengo la ubalozi wa Ujerumani na kushambulia baadhi ya mali na kuichoma moto bendera ya Ujerumani kisha kuweka ya kiislamu kabla ya kulichoma moto jengo hilo.