Saturday, September 15, 2012

Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 Usiku , ndani ya Uwanja wa Jamuhuri Dodoma



Popout

 
 Pichani juu na Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Linah kutoka THT akitumbuiza jukwaani usiku huu wakati wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012 likiendelea usiku
 
 Pichani juu na chini ni msanii anaetamba katika miondoko ya R&B hapa bongo,aitwaye Ben Paul akiwarusha wakazi wa mji wa Dodoma waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta linaleondelea usiku huu kwenye uwanja wa Jamuhuri.
 

 
 Msanii wa bongofleva aitwaye Shetta akiwaimbisha washabiki wake usiku huu.
 
  Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Rich Mavoco akiwaimbisha washabiki wake kibao waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 linalofanyika usiku huu ndani ya uwanja wa Jamuhuri.
 
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Dayna akijitokeza kwa mbwembwe jukwaani usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 linaloendelea hivi sasa kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma,ambapo wakazi wake wamejitokeza kwa wingi kuwashuhudia wasanii mbalimbali wanaotumbuiza kwenye jukwaa hilo.
 
 Wakazi wa mji wa Dodoma wakiwa wamejitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,ndani ya uwanja wa jamhuri mjini Dodoma.
 
 mmoja wa wasanii chipukizi katika anga ya muziki wa kizazi kipya,ambaye pia aliibuliwa na shindano la Serengeti Supa Nyota kutoka jijini Mwanza,aitwaye Young Killer akikamua jukwaani mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Dodoma usiku huu.
 
 Wasanii kutoka THT wakitumbuiza jukwaani usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
 
 Anaitwa Recho kwa jina la kisanii kutoka nyumba ya Vipati THT,akiimba jukwaani kwa madaha kabisa,huku umati wa watu (haupo pichani) ukishangilia kwa nguvu.
 
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya akiwa amebebwa juu  mara baada ya kujitokeza jukwaani na wasanii waliopa  mtafu kutoka THT.
 
Kwa hakika wakazi wa mji wa Dodoma wamejitokeza kwa wingi usiku huu kwenye uwanja wa Jamuhuri,ambako ndiko tamasha la Serengeti Fiesta 2012 likiendelea hivi,shangwe tuu.