Thursday, September 27, 2012

SUDAN KASKAZINI NA KUSINI HATIMAYE ZAFIKIA MAKUBALIANO KUHUSIANA NA SUALA LA MAFUTA.




Viongozi wa nchi za Sudan kaskazini na Sudan Kusini wamefikia makubaliano yenye vipengele tisa kuhusu baadhi ya tofauti zao, lakini wameshindwa kumaliza mzozo juu ya jimbo la Abyei na suala la ukomo wa mipaka ya mataifa yao.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amesema kuwa nchi hizo zitasaini “Itifaki ya Uhusiano” leo hii.
Msemaji wa Sudan Kusini Atif Kiir amesema kuwa Rais Omar Hassan al-Bashir wa Sudan na rais Kiir wamekubaliana juu ya masuala ya kiuchumi na kuundwa kwa ukanda maalumu usioruhusu shughuli za kijeshi katika eneo la mpaka baina ya mataifa hayo.
Ameongeza kuwa hatua hiyo ni ili kuruhusu shughuli za usafirishaji mafuta.
Kiir amesema kuwa usafirishaji wa mafuta ambao Sudan iliusitisha mapema mwaka huu, utarejea tena na kwamba ni masuala ya kiufundi tu ndiyo yaliyosalia kuanza upya kwa zoezi hilo.