Friday, September 14, 2012

PICHA ZA MATUKIO TOFAUTI WAKATI WA ZIARA YA MH. PINDA WILAYANI MAGU.



 
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akifungua gati la kupokelea samaki katika kijiji cha Kigangama wilayani Magu akiwa katika ziara ya mkoa wa Mwanza.
 
 Mtoto akiwa amenyanyuliwa juu ili aweze kumwona Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Sabasaba Mjini Magu.
 
 Shamba la kilimo cha umwagiliaji cha Mbogamboga la Ngongoseke lililoko katika kijiji cha Nsola wilayani Magu ni mfano wa kuigwa katika matumizi ya ziwa Victoria. Pichani, nyanya ndogondogo maarufu kwa jina la nyanyapori zikiwa zimelimwa kitalaam kwenye shamba hilo ambalo, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alilitembelea (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).