LEO Majira ya saa Mbili za asubuhi jumla ya watahiniwa 894,881 wanatarajia kuanza mtihani wao wa kumaliza elimu ya msingi wakiwa na matumaini ya kufanya vizuri na kuvuka salama kipimo hicho ambacho kitatoa tathmini ya kile ambacho wamekuwa wakikifanya kwa kipindi cha miaka saba.
Pilika za kufanya mtihani huo katika wilaya ya Mbeya Mjini zimeanza tangu majira ya saa 10 usiku hii leo katika maeneo ya Polisi Central mkoa wa Mbeya ambapo magari ya kuwasambaza wasimamizi wa mtihani wa Darasa la Saba walipoanza kupandishwa kwenye magari maalum.
Wakati hayo yakichomoza serikali ya kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imetoa onyo kali kwa watakaojaribu kufanya udanganyifu au waliozoea kufanya vitendo vya udanganyifu katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka huu kutothubutu kufanya hivyo.
|