Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa katika mazungumzo na Spika mpya wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Magareth Zziwa alipomtembelea leo Ofisini Kwake leo. Mhe. Zziwa alimtembelea Mhe. Makinda kwa lengo la Kujitambulisha baada ya kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mapema mwezi Julai.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimkabidhi Zawadi Spika mpya wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Magareth Zziwa mara baada ya kufanya nae mazungumzo leo ofisini kwake.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akifurahia Zawadi ya kikapu chenye zawadi mbalimbali mara baada ya kukabidhiwa na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Magareth Zziwa leo Ofisini kwake. Mhe. Zziwa alimtembelea Mhe. Makinda kwa lengo la Kujitambulisha baada ya kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mapema mwezi Julai.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa katika Picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Magareth Zziwa (Katikati) na Mbunge wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania Mhe. Angela Kiziga mara baada ya kumtembelea Mhe. Makinda Ofisini kwake leo.
Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge
Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge