Wednesday, September 19, 2012

GWIJI WA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA COLOMBIA AKAMATAWA NCHINI VENEZUELA.



 
Daniel Barrera a.k.a “  Crazy Barrera”
Mmoja kati ya wanaoaminika kuwa magwiji wa biashara ya dawa za kulevya nchini Colombia amekamatwa huko Venezuela.
Gwiji huyo Daniel Barrera maarufu kwa jila la “ Crazy Barrera” amekamatwa huko San Cristobal kukatiza mpaka kutoka Colombia kwa msaada wa mashirika ya Usalama ya Venezuela, Uingereza na Marekani.
Rais Juan Manuel Santos wa Colombia amemuelezea Barrera kuwa huenda ndie kinara aliyekuwa akitafutwa kuliko wote katika miaka ya hivi karibuni.
Colombia ni moja kati ya nchi wazalishaji wakubwa wa Cocaine duniani.