Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akiwapa nasaha wanamichezo (hawapo pichani) wa wizara hiyo katika tafrija fupi ya kuwaaga wawakilishi wa wizara hiyo ambao watashiriki katika mashindano ya Shirikisho ya Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (Shimiwi) iliyofanyika wizarani hapo jijini Dar es Salaam leo. Mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza mjini Morogoro kesho. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mwamini Malemi pamoja na Katibu wa Michezo, Jarahi Kilemile.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI. 21 DISEMBA, 2012.
0754 777478, 0714 809480.
|