Mbunge Msigwa (mwenye magongo) akisalimiana na wadau mbalimbali wa Usalama Barabarani, baada ya kuwasili katika Uwanja wa Samora mjini Iringa, kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa, Salim ‘Asas’ Abri (kulia) Mmiliki wa Blogu hii Father Kidevu (mwenye kofia) na Mdau Frank wa mjini Iringa. Pia Mbunge wa Viti Maalum(CCM) Mkoa wa Iringa, Ritha Moto Kabati nae alipata wasaa wa kutembelea maonesho hayo.
Licha ya kuwa Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini (CHADEMA) Rev. Peter Msigwa kuuguza mguu wake kulia uliotenguka lakini alipata wasaa wa kuungana na wananchi wa jimbo lake na taifa kwa ujumla kutembelea mabanda ya Maonesho yaliyopo katika Uwanja wa Michezo wa Samora mjini Iringa kujionea shughuli mbalimbali za Jeshi la Polisi na Vikosi vingine na mabanda ya wadau wa Usalama Barabarani yaliyopo uwanjani hapo katika maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa yanayofanyika Mkoani Iringa ndani ya Jimbo lake. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA”.
Mbunge Msigwa alisalimiana na watu mbalimbali wa eneo la Mlendege waliomlaki mara baada ya kuwasili.Picha na Mh. Peter Msigwa Blog