Thursday, September 20, 2012

MAREKANI YATOA DOLA MILIONI 1 KUISAIDIA TANZANIA KUIMARISHA MFUMO WA ULINZI BAHARINI.


 

Mkuu wa Mipango na Maendeleo(JWTZ) Maj. Gen. Le Mndeme akikata Utepe akishuhudiwa na Balozi wa Marekani Bw. Alfonso E. Lenhardt, kushoto Kamanda mkuu kikosi cha wanamaji NAVY Maj.Gen. Said Shaban Omary.

 

Balozi wa Marekani Bw.Alfonso Lenhardt akihutubia wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.

 

Meneja wa programu US Navy Bw.Steve Poland akikabidhi vyeti mmoja kati wahitimu wa mafunzo.

 

Balozi wa Marekani Bw Alfonso Lenhardt akisalimiana na maafisa wa jeshi la wanamaji Tanzania -NAVY.

 


Serikali ya Marekani imetoa msaada wa kuimarisha Mfumo wa Ulinzi baharini wenye thamani ya dola za Marekani milioni 1 ikiwa ni mafunzo pamoja na vifaa.

Balozi wa Marekani nchini Tanzania Alfonso Lenhardt ameshiriki katika hafla ya kukata utepe wa kufungua mafunzo pamoja na msaada huo katika kambi ya Kigamboni Wanamaji ya Kigamboni ya TPDF jijini Dar es Salaam.

Msaada huo kwa ujumla utasaidia ushirikiano wa kupata taarifa miongoni mwa Mamlaka za Bandari, askari wa majini na Jeshi la Wananchi wa Tanzania ikiwa ni kuongeza usalama majini.

Kwa hisani ya MO BLOG TEAM