Mabingwa Wa Afrika Mashariki Na Kati-Yanga Walala 3-0
Dar es Salaam Young Africans wameendeleza mwanzo mbaya wa Ligi Kuu Tanzania bara baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-0 toka kwa wakata miwa Mtibwa Sugar. Wakati huo Mnyama ameendelea kuunguruma uwanja wa Taifa baada kuichapa JKT Ruvu 2-0 Kwa mabao ya Amri Kiemba na Haruna Moshi Boban, pamoja na kucheza pungufu baada ya Emmanuel Okwi kupewa kadi nyekundu kipindi cha kwanza.