Promota wa ngumi za kulipwa nchini KAIKE MFAUME SIRAJU amewafanyia kitendo si cha kiungwana mabondia chipukizi Issa Omar na Mwaite Juma kwa kuwapambanisha tarehe 15/7 /2012 kwa makubaliano ya kuwalipa kama ilivyo kawaida na badala yake kutowalipa mabondia hao chipukizi
Tarehe25/06/2012 aliwasainisha mkataba mbele ya katibu mkuu wa ngumi za kulipwa Tanzania Ibrahim kamwe kuwa Issa omar kucheza na Ramadhan kumbele kwa malipo madogo ya 80,000/=(elfuthemenini), alikadhalika kwa mwaite juma kucheza na Anthony Mathias. Vijana walicheza na hawakulipwa.baada ya pambano alitoroka, Walipojaribu kumdai haki yao kwa siku zilizofuatia walipigwa kalenda na kuwatembezatembeza kwa usumbufu kwa kuwaambia wamfate mara mango garden asubuhi na kuwagandisha mpaka jioni na kuwaambia njooni kesho magomeni saa tano vijana walifika saa tatu na kuganda mpaka saa tisa walipompigia simu aliwaambia waachane nae wakati mwanzo alikuwa anawaambia wamsubiri sasa anawaambia waachane nae na kuwatisha.
Vijana waliripoti kwa katibu mkuu Ibrahim kamwe nae akampigia simu kaike,nae kaike akakubali kuwalipa kupitia ibrahim hivyo wasimfatefate,matokeo yake anamzungusha katibu mara hivi mara vile hadi mwisho anadiriki kusema kwanza wale watoto tu wasituzingue inaonekana hana nia ya kuwalipa vijana hao. Nikiwa kama kiongozi nikajaribu kumuelimisha kaike kuwa umeingia mkataba na mabondia wa kuwalipa baada ya pambano hivyo yakubidi kuwalipa ili wajitahidi kwa kujua wana ajira ya uhakika na kujitahidi kwao ni manufaa yetu na taifa kiujumla, ukizingatia siku hiyo ya mchezo yule bondia mwingine aliumia sana jicho na wazazi wake kulalamika kwa uongozi tunachezesha mabondia bila ya kuwalipa na hatuwajali wanapoumia.
Mambo yanayofanywa na kaike si ya kiungwana ni kuwavunja moyo mabondia mabondia chipukizi,kudumaza ngumi na kufanya mchezo wa ngumi uonekane ni mchezo wa wahuni kwa vitendo vya kihuni kama hivi.Halafu wanamasumbwi ulalamika hatupati wafadhili wakati uaminifu haupo baina yetu wenyewe.
regards
ibrahim kamwe
+255 713 501991
+255 784 501991
+255 767 501991
ibrakamwe@yahoo.com