Tuesday, September 18, 2012

Maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama kitaifa yaendelea mjini Iringa



 
Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalkama barabarani leo yameingia siku ya Pili ambapo kitaifa yanafanyika mjini Iringa katika Uwanja wa Sokoine na kushirikisha wadau mbalimbali wa Usalama barabarani. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA”. Pichani ni Meneja Masoko na Utafiti wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) akitoa maelekezo kwa vijana na watoto waliofika bandani hapo leo.
 
Miongoni mwa washiriki wa Maonesho ya mwaka huu ya wiki ya Nenda kwa Usalama ni Kampuni ya ASAS ambao mbali na shughuli za usafirishaji wa mizigo pia ni wazalishaji wakubwa wa Bidhaa za Maziwa ambayo asilimia kubwa hupatikana kutoka katika mashamba ya mifugo ya ASAS DAIRY FARM yaliyopo mkoani Iringa. Ng’ombe wa kisasa, Mbuzi, kondoo, Ngamia na Farasi ni miongoni mwa mifugo inayofugwa katika mashamba hayo.
Pichani ni baadhi ya wananchi wa mjini Iringa wakiwa katika banda la ASAS Dairy Farm wakiangalia Ngombe, Farasasi, Nyati na Ngamia waliopo katika maonesho hayo leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA”.
 

Wananchi wa mjini Iringa wakiwa katika banda la ASAS Dairy Farm wakiangalia Nyati (Mbogo Maji)  waliopo katika maonesho hayo leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA”.
 
Watoto wa mjini Iringa wakiwa katika banda la ASAS Dairy Farm wakiangalia  Ngamia waliopo katika maonesho hayo leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA”.
 
Wananchi wa mjini Iringa wakipata maelezo mbalimbali kutoka kwa mmoja wa maofisa wa TANROADS walipotembelea katika banda hilo lililopo pamoja na Wizara ya Ujenzi. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA”.
 
Watu mbalimbali wakiwa katika Banda la Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wakiangalia gari maalum la kufundishia madereva lililopo bandani hapo.
 
Watoto ndio umri sahihi kutoa mafunzo ya namna ya matumizi sahihi ya barabara. Na iwapo kama watoto hawa watapata elimu ya kutosha juu ya utumiaji wa barabara itachangia kwa kiwango kikubwa yatachangia kupunguza kiwango a ajali za barabarani miaka ijayo. Hapa watoto wakimsikiliza ofisa wa Wizara ya Ujenzi.
  
 Wananchi wa mjini Iringa wakipata maelezo mbalimbali kutoka kwa mmoja wa maofisa wa Wizara ya Ujenzi walipotembelea katika banda hilo jana. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA”.
 

Wananchi wa mjini Iringa wakipata maelezo mbalimbali kutoka kwa mmoja wa maofisa wa Jeshi la Polisi walipotembelea katika banda hilo lililopo katika viwanja vya Samora mjini Iringa yanapofanyika maonesho ya maadhimisho ya wiki ya Nenda kwa Usalama kitaifa. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA”.
 
 
 Mara nyingi zinapotokea ajali Hospitali huwajibika kwa kiwango kikubwa kuhakikisha afya za watu zipo zinarejea katika hali ya kawaida na kuendelea na shughuli za ujenzi wa taifa. Katika Maonesho ya mwaka huu ya wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani kitaifa mjini Iringa, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa wanashiriki na hapa watu mbalimbali wakipata ushauri na kuangaliwa afya zao. Nenda kwa Usalama kitaifa. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA”.