Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbles Lema.
Na Datus Boniface
JAJI Mkuu wa Tanzania Othuman Chande, ataongoza jopo la majaji watatu katika kutoa hukumu ya rufaa ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbles Lema, leo inatarajiwa kutolewa hukumu katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.
Lema (Chadema), alivuliwa Mbunge Mahakama kwa kile kilichoelezwa kuwa ni ukiukaji wa taratibu za uchaguzi, ikiwemo matumizi ya Lugha za matusi.
Hukumu ya leo ni mwendelezo wa rufaa yake ambayo Lema aliitaka kupinga kuvuliwa ubunge.
Katika rufaa hiyo Jaji Mkuu atawaongoza Jaji Salum Masati na Mh.Jaji Natalia Kimaro.