Thursday, September 20, 2012

Taswira:Hatua kwa hatua Jinsi Matokeo ya Uchaguzi Mdogo Bububu Zanzibar Yalivyopatikana



  Mshindi wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Bububu Husein Ibrahim Makungu (BHAA) akionesha cheti chake cha ushindi baada ya kutangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kuwa mshindi wa Uchaguzi huo.
 Mshindi wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Bububu Husein Ibrah Makungu(BHAA) akitoa shukrani kwa ushindi wake na kuwapongeza wapiga kura wake kwa kumpa ushindi ili kuliongoza jimbo hilo kwa maendeleo ya Wananchi wa Jimbo hilo.
   Msimamizi wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Bububu akimkabidhi Cheti mshindi wa uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi Hussein Ibrah Makungu, baada ya kutangaza matokeo ya uchaguzi huo katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa SUZA Betras.
 mwonekano wa matokeo
   Maofisa wa Uchaguzi Mdogo Jimbo la Bububu wakijumuisha kura katika kituo cha kujumlishia kura zote kilichokuwa katika Chuo cha Taifa SUZA Betras.
  Msimamizi wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Bububu akitoa matokea ya Uchaguzi katika Ukumbi wa Chuo cha Taifa SUZA,Betrais Betrais
 Mgombea wa Chama cha Mapinduzi Hussein Ibrahim Makungu na Viongozi wengine wa Vyama vilivyoshiriki Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Bububu wakifuatilia matokeo ya Uchaguzi.
  Viongozi wa Vyma vya Siasa wakifuatilia Matokeo ya Uchaguzi.
 Wasimamizi wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Bububu kutoka Nje wakifuatilia Ujumlishaji wa Kura katika chumba cha kujumlishia Kura Betras.
 Kiongozi wa Chama cha Wakulima Mchenga, akitowa shukrani kwa nia ya Mgombea wake hakufika katika chumba cha kutolea matokeo.
  Aliyekuwa Mgombea wa Uchaguzi jimbo la Bububu kwa tiketi ya Chama cha CUF, Issa Khamis Issa, akitowa malalamiko yake kutokana na kushindwa kwake na Mgombea wa CCM,Hussein Ibrahim Makungu(BHAA) baada ya kutangazwa mshindi wa Uchaguzi huo. katika ukumbi wa Chuo cha Taifa cha SUZA Betras.
Mgombea wa Chama cha ADC Zuhura Bakari Mohammed, akitowa shukrani kwa wananchi waliompigia kura katika uchaguzi huo, baada ya kutolewa matokea ya uchaguzi wa Bububu.