Friday, September 21, 2012

Hii ndo filamu mpya ya kanumba, miezi 6 baada ya kufariki.


Kwa mara ya kwanza toka kifo chake April 7 mwaka huu filamu mpya ya Marehemu 'Steven Charles Kanumba' inatarajiwa kuingizwa sokoni na kampuni ya usambazaji ya Step Entertainment ya hapa nchini. Filamu hiyo itakayokuwa ikifahamika kwa jina la ndoa yangu ndania yake yuko mhusika mkuu mwingine 'Jackline Wolper' ambayo kwa maelezo ya Step wanadai filamu hiyo imetengenezwa kwa kiwango cha juu ambapo haiwezi kukopiwa kirahisi na
maharamia wa filamu.Filamu hiyo inatarajiwa kuingia sokoni mwishoni mwa mwezi Septemba mnamo tarehe 28 na wapenzi wa msanii huyo aliyetamba sana kwenye ulimwengu wa filamu Tanzania na hata Duniani watakuwa na uhakika wa kumuona staa huyo kwenye filamu hiyo mpya.