CUF Chama cha wanachi kinalaani kitendo cha wafuasi wa CUF kupondwa mawe na wafuasi wa CHADEMA walipokuwa wakiendelea na shughuli kutangaza mikutano inayoendelea Arusha . Chama cha wananchi CUF kinasikitishwa nakulaani kitendo cha viongozi wa chadema mkoani Arusha kuwashawishi wafuasi wao kuwaponda mawe wanachama wa CUF wanaoendelea na mikutano ya kisiasa inayofanywa na CUF tangu mwanzo wa wiki hii.
Hii imedhihirishwa na maeno na Godbless Lema juzi alipokuwa waapowahutubia wafuasi wa Chadema kwenye viwanja vya Stendi ya Nduruma alisema kwamba CUF wametuvamia na kuwasihi ile slogan ya “kamata mwizi men” sasa ianze.
Na ushahidi tuanao. Hata hivyo wameshawishi vijana kugawa kiwanja vya Levorosi stendi ya Nduruma kwa kisingizio kwamba wanataka kuweka meza za biashara kiwanja ambacho CUF tuantegemea kufanya mkutano wa hadhara siku ya Jumapili.
Leo asubuhi wanachama wa CUF wamepondwa mawe walipokuwa mtaa wa Kilombero kata ya Levorosi. Kutokana na vurugu hilo gari la matangazo la CUF limepondwa mawe na mwanachama mmoja aitwaye Athuman Abdurahman alipigwa jiwe jichoni na taarifa tumezifikisha polisi. CUF kinaona Chadema kama chama kisichoweza siasa za ustahimilivu,hawajiamini na bado ni wachanga kisiasa.Hii inadhirishwa na kutoelewa maana ya demokrasia na uhuru wa Mtanzania kuamua kujiunga na chama chochote atakacho.
Bado hawajakomaa kisiasa kama jinsi CUF ilivyokaomaa kisiasa hatukudhuru chama chochote wanapofanya siasa maeneo mbalimmbali hapa nchini. CUF inatoa onyo kali kwa viongozi wa Chadema kwamba hali hii ikiendelea wajue hawataweza kufanya shughuli zao sehemu yoyote Tanzania kwani uwezo wa kuwafanya tutakavyo tunao na kwasababu wameanza tuanaweza kumaliza.Ile NGANGARI kwa polisi tunaweza kuwahasishia wao wakose pa kukaa, ila hatupendi tufikie huko na kama wanabusara na ni wanasiasa kweli wenye nia ya kutumia hoja badala ya vurugu kumkomboa mtanzania watafakari hilo.
CUF inaendelea kusisitiza tutaendelea na shughuli za kisiasa mkoani Arusha hakuna wa kutuzuia na tutaendelea Oparesheni MCHAKAMCHAKA na mikutano itaendelea kufanyika na kama wao ni wababe kweli na wanatumia hoja ya vurugu waendelee na mipango yao ya hujuma na tutawafundisha siasa kwani bado hawajakomaa.
Imetolewa na:-
Naibu Mkurugenzi wa Habari ,Uenezi na Haki za Binadamu CUF.
Mh.Abdul Kambaya
Simu:0719566567