Bw Mwakalebela
Hatua ya NEC ya CCM Taifa kumteua Bw Frederick Mwakalebela kuwa miongoni mwa wagombea 10 wa nafasi 5 za ujumbe wa mkutano mkuu wa Taifa kuwakilisha wilaya ya Iringa mjini ni moja kati ya hatua za kumwezesha Mwakalebela kuanza kujipanga kwa ajili ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 iwapo wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM wilaya ya Iringa mjini leo watampitisha katika nafasi hiyo aliyoomba.
Mwakalebela ni mmoja kati ya wana CCM ambao wameonyesha uvumilivu mkubwa ndani ya CCM pamoja na kuchakachuliwa katika kura za maoni mwaka 2010 baada ya kushinda nafasi hiyo na kupokonywa na NEC na kumpa Monica Mbega ambaye alishindwa na mchungaji Peter Msigwa (Chadema).
Hivyo kosa ambalo lilifanywa na NEC chini ya mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete Dodoma kwa kuengua jina la Mwakalebela katika kinyang'anyiro sasa limefutika kwa CCM kusita kurudia kosa hilo.
Mwakalebela mbali ya kugombea nafasi hiyo kwa ngazi ya wilaya kwenda Taifa bado ni mgombea wa nafasi ya uchumi ya mkoa wa Iringa uchaguzi utakaofanyika hivi karibuni.
Mtandao huu unamkakia ushindi mwema Bw Mwakalebela katika uchaguzi wa leo na ujao